Song Page - Lyrify.me

Lyrify.me

Dingi by LocalModel93 Lyrics

Genre: rap | Year: 2019

Ukitaka kuwa dingi, 
Lazima uishi kama mimi
Uvunje makundi ya kipimbii
Ishi kama dingi, 
Usiwaze magari
Waza mali, 
Natamani nirudie fani
Niandike kama zamani
Ila haiwezekani wife ukishamuweka ndani
Nasema hiwezekani
Dingi kuwa mtumwa wa shetani
Haiwezekani dingi kuwa na mamanzi wa pembeni
Haitakikani dingi kudakwa ugoni
Dingi unaanza kumsoma usoni
Dingi unaanza kumuona nguoni
Dingi hawezi vaa hereni maskionii
Dingi mara nyingi huwezi kumkuta jikoni
Maaa .... Dingi hatumwi sokonii..
Dingii .. *3 anachonga mambo ya msingi
Dingi sio lazima kuwa na watoto shule ya msingii
Dingi huwa apendi sanaa kulamba chumvi, wazee wa chumvini hamuwezi kuwa madingiii
Babaa Heaven,Niite babaa Dominaa
Dingi lazima umpe wife heshima
Dingi sio kima, sometimes anakupima
Dingi lazima uwe na Hekima
Vinginevyo watoto watakusunyaa
SharaOut kwa mwanangu King'onde Sunyaa
Dingi ndio anajua kuzaa sio kunyaa
Dingi mtoto akizaliwa lazima umpe jina
Umfunze kujitumaa, Dingi ndio anamjengea mwanae heshimaa
Dingi sio kodingoo, Hapigi gongo
Anachapa fimboo, Dingi anacheza kwaya sio Bolingo
Dingi anaweza kutoa chongo, kama unaakili za Pongo, Dingi kama kadinali Pengo, Sometimes dingi anatoa pepo
Anakemea watoto , pamoja na kuwalea kwa upendoo, Dingi huwa na matumaini makubwa yakuiona pepo, Anapambana kwa bidii kuitengeneza kesho
         ___Your__Author__
                Lekule_Rongai___
                  (LocalModel93